14 Agosti 2013 - 19:30
Zimebaki siku chache waasi wasambaratishwe

Kushindwa Marekani na nchi za kimagharibi kuondoa utawala wa Bashar Alasad, serikali ya Syria kutangaza ushindi mnamo siku chache zijazo kulingana na kusambaratishwa vibaya waasi wa nchi hiyo na kukosa sehemu ya kukimbilia.

Ripoti ya ABNA- Waziri mkuu wa Syria Wael al-Halqi amesema zimebaki siku chache tu kabla ya makundi ya waasi kusambaratishwa, huku upinzani ambao unaungwa mkono na nchi za magharibi ukiendelea kutoa madai yao ya zamani ya kutaka serikali iondoke madarakani ikiwa ni kama utangulizi wa mwongozo wa kumaliza mgogoro wa muda mrefu. Bw Al-Halqi amefafanua kuwa nchi hiyo inakabiliwa na vita ya kijeshi, kiuchumi, vyombo vya habari na kisiasa vinavyojaribu kulenga mfumo wa serikali na umoja wa watu wake. Amezilaani nchi za magharibi zinazounga mkono upinzani na kusema nchi hizo zimeamua kulenga uchumi wa nchi hiyo baada ya kutumia silaha zao na kushindwa kupata ushindi.